HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 11, 2011

Redd's Yazungumza na Warembo wa Miss Tanzania jijini Dar leo

Meneja wa kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro akizungumza na warembo watakaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakati alipowatembelea katika hoteli ya Girrafe Ocean View,Kunduchi jijini Dar es salaam leo.kulia ni Mshauri Nasaha kwa warembo hao,Sussane Mrema.
 Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao leo.
Mshauri Nasaha,Bi. Sussane Mrema au Bi. Suzie akitoa ushauri nasaha kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakati Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original alipokuwa akizungumza na warembo hao leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View,Kunduchi jijini Dar.
Meneja wa kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro akiwakabidhi zawadi ya mashati ya Redd's baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View,Kunduchi jijini Dar.
Warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad