HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 29, 2011

Futari Mji wa Reading

picha ya pamoja na wanajumuia

Asalaam Aleykhum,

READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) Iliandaa futari maalum leo jioni 28.8.11 na kuwaalika wanajumuia mbalimbali kutoka Reading, London, Coventry na sehemu nyingine ili kupata futari kwa pamoja. Hii ni desturi ambayo hufanyika kila mwaka wakati huu wa mwezi mtukufu ramadhani. Lengu kuu haswa ni kujumuika pamoja katika kudumisha upendo, amani na umoja kwa wana jumuia pamoja,kuzingatia yale yote yalio mema na kukataza yalio Mabaya.

Mgeni Rasmi wa siku ya leo alikuwa Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na baadhi ya maofisa wa ubalozi wetu wa Tanzania Hapa London.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa REACO Said Mahmud tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioitikia mwito na kuja kujiunga nasi. Tunawashuru sana.

Kwa maelezo au mawasiliano zaidi tafadhali tutumie email ifuatayo, reaco@hotmail.co.uk

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE
  Baadhi ya Viongozi wa REACO katika Picha ya pamoja.
Mh Chabaka akifurahia jambo wakati Afisa wa UBalozi Kiondo akiteta na Ustaadhi Sungura.
Mh Naibu Balozi Chabaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa REACO.
Baadhi ya viongozi wa REACO wakipata Futari
 wanajumuia pamoja na wageni wakipata Futari kwa pamoja.
Watoto Wakipata Futari.
Mh. Naibu Balozi akipata Futari na Wadau.

1 comment:

  1. Hayo ni makundi ya watu ambao wanatuabisha Waafrika kusingizia kuwa nchi zao zina matatatizo ilİ wapewe matunzo ya bure,chakula bure,nyumba bure ati wakimbizi wa kisiasa.AIBU KUBWA.Mbona sisi huku nyumbani tunaishi kiheshima.Waafrika tutapenda vya dezo mpaka lini?

    ReplyDelete

Post Bottom Ad