HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 29, 2011

KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC,MCC na CCBRT watoa huduma ya afya bure,Moshi

Mmoja wa madaktari wa shirika la MCC akitoa huduma ya afya kwa mmoja wa watoto waliofika katika kituo cha afya cha mtakuja kwa ajili ya matibabu.
Mratibu wa mradi wa huduma za afya kijijini humo,Bw Gerbert Ricks akizungumza na wanahabari (hawako pichani)kushoto kwake ni Bi Iris van de Gevel,mratibu kutoka shirika la MCC.
Baadhi ya watoto wengine wakiwa wamesindikizwa na wazazi wao,wakijiandikisha kwa ajili ya kupatiwa huduma ya afya iliyotolewa na shirika la huduma kwa watoto la Uholanzi(MCC) likishirikiana na kwanda cha sukari cha TPC na kituo cha huduma za walemavu cha CCBRT.
Baadhi ya watoto wengine wakiwa wamesindikizwa na wazazi wao,wakijiandikisha kwa ajili ya kupatiwa huduma ya afya iliyotolewa na shirika la huduma kwa watoto la Uholanzi(MCC) likishirikiana na kwanda cha sukari cha TPC na kituo cha huduma za walemavu cha CCBRT.
Kaimu afisa mtendaji utawala wa TPC,David Shilatu akizungumza na wanahabari juu ya huduma ya afya iliyotolewa na shirika la huduma kwa watoto la Uholanzi(MCC) likishirikiana na kiwanda cha sukari cha TPC
na kituo cha huduma za walemavu cha CCBRT.
Mtaalamu wa magonjwa ya meno wa hosptali ya TPC Pius Tarimo akitoa maelekezo kwa mmoja wa wagonjwa waliofika kupata matibabu katika kambi ya wiki moja ya huduma ya afya iliyotolewa na shirika la MCC wakishirikiana na kampuni ya sukari ya TPC na kituo cha huduma za walemavu cha CCBRT.
Mmoja wa wagonjwa waliofika katika kituo hicho kupata matibabu ,hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana mara moja.Picha/Habari na Dixon Busagaga,Moshi

KIWANDA cha sukari TPC Ltd kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali ya huduma za afya kwa watoto la Uholanzi (MCC) na kituo cha huduma za watu walemavu cha CCBRT wametoa huduma za matibabu kwa watoto zaidi ya 1000 katika kijiji cha Mtakuja wilayani Moshi vijijini.

Kaimu afisa mtendaji utawala wa TPC,ndg David Shilatu amesema kuwa matibabu hayo kwa magonjwa ya aina mbalimbali ukiwemo ukimwi yametolewa kwa siku saba katika kijiji hicho na kuhusisha watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano hadi Tisa wilayani humo.

Amesema mbali na huduma za matibabu lakini asasi hizo kwa pamoja wamekuwa wakiwasaidia wananchi wa vijiji vinavyozunguka kiwanda hicho kwa kuwasaidia utoaji wa huduma katika miradi ya Elimu,Kilimo na Miundombinu.

Ndg Shilatu amesema wagonjwa walioonekana kuhitaji matibabu zaidi walipelekwa katika hospitali ya kiwanda cha TPC huku wengine watakaoshindikana watapelekwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi.

Amesema kiwanda kimeamua kusaidia jamii inayozunguka kiwanda hicho kama njia moja wapo ya kuboresha mahusiano na wananchi ili wanufaike na uwepo wa kiwanda katika kuwakomboa katika masuala mbalimbali.

Awali mratibu wa mradi wa huduma za afya kijijini humo,Ndg Gerbert Ricks amesema tangu wamekuwepo kwa siku saba kijijini hapo wamewapima watoto wao magonjwa mbalimbali ikiwemo Malaria, Naimonia, utapiamlo, HIV,wenye matatizo ya ukubwa wa kichwa na wale wenye midomo iliyopasuka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad