HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 7, 2011

YANGA YATINGA NUSU FAINALI KWA MIKWAJU YA PENATI 6-5

 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Keneth Asamoah (kushoto) akichuana vikali na Beki wa timu ya Red Sea ya Eritria katika mchezo wa robo fainali ya Mashindano ya Kagame-Castle Cup uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penati 6-5.
 Kiggi Makasi wa Yanga (kushoto) akipambana na Mchezaji wa timu ya Red Sea,Aron Zekarias.
 Mshambuliaji wa Yanga,Davies Mwape (kulia) akijaribu kutaka kumtoka kiungo wa katikati wa timu ya Red Sea ya Eritria,Yakob Tekie wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kagame-Castle cup uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Kiggi Makasi wa Yanga akiruka daruga la beki wa timu ya Red Sea leo.
 Nyanda wa timu ya Yanga,Yaw Berko akiokoa moja ya penati.
 Kocha wa timu ya Red Sea ya Eritria,Efreim Tewolde akiongozwa na askari Polisi kutoka uwanja wakati walipokuwa wakimzonga muamuzi wa mchezo huo kwa madai kwamba aliipendelea timu ya Yanga mara baada ya kumalizika kwa mpira
 Wachezaji wa timu ya Red Sea wakiwazonga waamuzi wa mchezo huo.
 Wapiganaji Mzigoni.
Shangwe ilitawala uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad