HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 6, 2011

WAMACHINGA JIJINI MWANZA LEO WACHACHAMAA,WATAKA MPAKA KIELEWEKE

Jijini Mwanza leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi,kumezuka vurugu kubwa sana kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi jijini humo kwa madai ya kwamba wafanyabiashara hao kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.
Vibanda kadhaa vimevunjwa na Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
  Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza,Afande Simon Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.
hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.

kwa zaidi za tukio hili lililotokea huko Mwanza leo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad