![]() |
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Ummy Ally |
NA MAGRETH KINABO - DODOMA.
WANAUME wanaofanyiwa vitendo vya kikatili wameshauriwa wasiogope kwenda kuripoti katika vituo vya polisi ambapo vina madawati ya watu waliofanyiwa ukatili .
Wito huo, ulitolewa leo Bugeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Faida Mohamed Bakar (CCM) Chakechake lilioulizwa kuwa wanawake wanaofanyiwa vitengo vya ukatili wanaficha.
Akijibu swali hiyo Naibu Waziri huyo alisema alisema wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo wako wengi na hawafichi ila wanaume ndio wanaoficha.
Hata hivyo alimtaka mbunge huyo kuwasiliana naye baadae iliampe twakimu hizo kkwa kuwa suala hilo linajumuisha wadau mbalimbali.
Naibu Waziri huyo akijibu swali la Msingi Viti Maalum( CCM, Agnes Hokororo lililouliza kuwa je ni kwa kiwango gani serikali imetekeleza Mpango wa Kitaifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto(2001- 2015, pia ni wangapi waliotambuliwa na wangapi sheria imechukua mkondo wake.
Naibu Waziri huyo alisema utekelezaji wa mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali zikiwemo asasi zisizoza kiserikali ,Mashirika ya dini na taasisi za serikali.
Alisema kwa mujibu wa wa Tanzania Demographic and Suvery(TDHS) za 2010, twakimu zinaonyeshankuwa asdilimia 39 ya wanawake wenye umri wa miaka 15. Hivyo theluthi moja aua asilimia 33 ya wanawake hao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha mwaka 2009.
Aliongeza kuwa ukatili dhidi ya wanawake unajumuisha makosa mbalimbali ya jinai makosa haya yanaripotiwa polisi na mahakamani kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo alisema tatizo hilo halijaiisha katika jamii, hali halisi inaonyesha matukio yanazidi kuongezeka na juhudi za pamoja za serikali na wadau mbalimbali zinahitajika ili kutokomeza.
No comments:
Post a Comment