HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 18, 2011

Mkongwe Aisha Madinda atua Extra Bongo

Mkurugenzi wa Bendi ya Exta Bongo,Ally Choki akimtambulisha Mcheza Shoo Mkongwe,Aisha Madinda leo mbele ya waandishi wa habari
 Na Mwandishi Wetu.

MCHEZA shoo mkongwe na maarufu wa Bendi ya Muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda leo amejiunga rasmi na Bendi ya jirani ya Extra Bongo. 

Akimtambulisha kwa waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky alisema anafuraha sana kumpata mcheza shoo ambaye anamini ataleta mabadiliko ndani ya Extra Bongo kulingana na uwezo wake na  jinsi anavyomfahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari,Aisha Madinda amesema ameamua kuungana na wacheza shoo ambao anaamini akiwa nao katika safu hiyo atafanya vizuri na kipaji chake kitazidi kupanda juu zaidi. 

Aisha tayari ameshaanza mazoezi na atatambulishwa rasmi kwa mashabiki jumatno kwenye Klabu ya masai Ilala jijini Dar es Salaa.

Kiongozi wa wacheza Shoo, Super Nyamwela alimkaribisha Aisha kwa mikono miwili na kusema sasa kazi imekamilika na kuwataka wapenzi na mashabiki wajitokeze kwa wingi mara ya kwanza wanapomtambulisha Aisha pale klabu masai Ilala ndipo moto mkali wa Exra Bongo utaanza kuwaka.

1 comment:

  1. HONGERA KUHAMIA HUKO ANGALAU UTAPATA MSAADA WA KARIBU ZAIDI KWA HUYO SHOSTI WAKO MAANA MWENZIO ALIANZA MAPEMA,LAKINI CHOKI MBONA ULICHELEWA KUMSAIDIA MAPEMA? LAKINI HALIJAHARIBIKA JAMBO BORA MUPATE KUUGUZANA KWA KARIBU ZAIDI BIG UP EXTRA BONGO!!! KUMBUKA ASISAHAU KUMEZA DAWA ZAKE NA ASIJISAHAU KUKESHA KILA MARA AWE ANA PUMZIKA PUMZIKA MAANA MIGUU ISIJE VIMBA!!!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad