HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 20, 2011

Uzinduzi wa Video mpya ya Wasanii wa Bongo Flava inayohusu seherehe za miaka 50 ya uhuru Tanzania wafanika leo jijini Dar

Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki Tanzania (Tanzania Flava Unit),Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa video yao mpya inayohusiana na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,mkutano huu umefanika mchana huu,Leaders Club,jijini Dar.kushoto ni Mjumbe wa Chama hicho,Khadija Shaaban Keysher.
Msemaji Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Said Fella a.k.a Mkubwa Fella (shati la pinki) akiwatambulisha viongozi waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar.
Wasanii pamoja na waandishi wa habari wakiiangalia video hiyo.

Ifuatayo ni hotuba iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama Hicho,Hamis Mwinjuma

Ndugu zangu habari za mchana,

Nachukua fursa hii kuwakaribisha katika uzinduzi wa video ya wsanii inayohusiana na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, hii ni sehemu yetu na sisi ya kusherehekea kama vijana tukionesha kuguswa kwetu na hili, na wakati huo huo tukijaribu kuonesha mchango wetu kama vijana kwa serikali yetu ambayo kwa njia moja ama nyingine inahitaji shukrani, kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.

Tuna uhuru, tuna amani na mambo yanaenda ingawa matatizo ya hapa na pale yapo, lakini tumeangalia upande mzuri zaidi na tumeona kabisa huu ndio muda muafaka wa kukumbushana pale tuilipojikwaa, ili tupate kwernda kwa mwendo mzuri.

Katika miaka hii 50 ya Uhuru sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo zimeleta ajira kwa vijana. Unaweza kuona jinsi wasanii mbali mbali walivyojikwamua kupitia muziki, mifano hai imo hata humu ndani, watu wanaendesha magari, watu wanaishi kwenye nyumba nzuri na wana miradi yao kupitia muziki huu wa kizazi kipya.

Si vibaya basi kwa kile kidogo unachokipata kukitolea shukrani, kuonesha kwamba unakithamini, sisi twajivunia miaka 50 ya uhuru na tunahisi kwamba tuna kila haja ya kusherehekea.

Sisi kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.

Kwa fikra zetu hii ni muhimu, kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa burudani?

Hilo lilikuwa wazo la kwanza.

Lakini jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika, kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.

Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.

Video hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 30.

Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.

Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!

Hamis Mwinjuma
Mwenyekiti
Tanzania Flava Unit

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad