HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2011

UZINDUZI WA KILIMANJARO JIVUNIE UTANZANIA WAFANYA SANA LEO

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja akizungumza leo katika uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager ikiwa ni harakati ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Kampeni hii imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,katikati ya Jiji la Dar na kuhudhuriwa na wageni mbali mbali.
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche, Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo, Mjumbe wa Bodi Geoggrey Msella, Mkurugenzi Masoko TBL, David Minja na Maneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio wakiwa wameshika bia za Kilimanjaro Premium Lager kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya ‘Kili Jivunie uTanzania uliyofanyika katika Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goetzche akifafanua jambo juu ya Kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi leo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL,Emma Oriyo,akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania iliyofanyika leo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,jijini Dar.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu.
Wanandinga wa Zamani,Lunyamila na Salvatory Edward pia walikuwepo.
Carol Ndossi na Dorice Malulu.
 MC Taji Liundi akiwa Libenekeni leo.
 Wakuu wa TBL wakiwa katika mangumzo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo (katikati) pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions,Aggrey Maliale.
 Viongozi wa TBL wakimsikiliza MC wakati wa Shughuli hiyo.
 Mwanariadha mkongwe Nchini,Juma Ikangaa akibadilishana mawazo na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions,Aggrey Maliale.
 Mie nikiwa na Kaka yangu Taji Liundi pamoja na Mdau.
 Kiongozi wa Bendi ya Kilimanjaro,Waziri Ally akiteta jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad