HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 30, 2011

Serikali za Korea Kusini na Denmark zatoa msaada kwa Tanzania

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini msaada wa bilioni 318 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini wa ujenzi wa njia ya usambazaji umeme kutoka Iringa, Shinyanga na ujenzi wa Majengo ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili na maandalizi ya vitambulisho vya kitaifa. Kulia ni Balozi wa Korea kusini nchini Balozi wa Korea Kusini Young hoon Kim.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto ) akibadilishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 318 na Balozi wa Korea Kusini Young hoon Kim (kulia) leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa njia ya usambazaji umeme kutoka Iringa, Shinyanga , ujenzi wa Majengo ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili na maandalizi ya vitambulisho vya kitaifa.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini msaada wa bilioni 273 kutoka Serikali ya Denmark. Kulia ni Balozi wa Denmark nchini,Bjame Sorensen.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto ) akibadilishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 273 na Balozi wa Denmark nchini Bjarne Sorensen (kushoto) leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusaidia bajeti ya serikali, elimu na kuimarisha utawala bora nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad