HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 31, 2011

Dodoma wanyakua ubingwa wa Safari Lager Pool 2011

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kulia) akikabidhi kombe la ubingwa wa Taifa wa Mashindano ya Safari Lager kwa Nahodha wa Timu ya Pool ya mkoa wa Dodoma ambao ndio mabingwa wapya wa mchezo huo kwa mwaka huu.
Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni zawadi ya ubingwa wao huo walioupata usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo (kushoto) akikabidhi kitata cha sh. mil 3.5 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Ilala,ikiwa zawadi ya ushindi wa pili walioupaka mkoa huo.
Mwenekiti wa Chama cha Pool Taifa,Isaack Togocho akikabidhi kitita cha sh. mil 2 kwa kiongozi wa timu ya mkoa wa Mwanza ambao walishika nafasi ya tatu katika fainali hizo.
Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Mchezo wa Safari Lager Pool Taifa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene akiwa pamoja na viongozi wa mchezo wa Pool na viongozi wa TBL wakifuatilia moja ya michezo ya Fainali za Pool za Taifa kati Ilala na Dodoma iliyokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Kilimani,Mjini Dodoma Usiku wa Kuamkia leo.
 Mashabiki lukuki walifurika kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma kushuhudia fainali za Safari Lager Pool kitaifa zilizomalizika usiku wa kuamkia leo.
Mratibu wa Mashindano ya Pool,Innocent Melleck akitoa taratibu ya kutolewa kwa zawadi za washindi wa mashindano hayo.
Shangwe ilitawala kwa mashabiki wa timu ya mkoa wa Dodoma ambao ndio mabingwa wapya 2011.

Timu ya mkoa wa Dodoma ikiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad