HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 11, 2011

Rock City Marathon 2011 kufanyika septemba 4


Mratibu wa mashindano ya riadha yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2011’, Zaituni Ituja (kushoto) wa Kampuni ya Capitalplus International (CPI) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui na katikati ni Mkurugenzi wa Maliasili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahim Musa aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wake Ezekiel Maige.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano ya Rock City Marathon 2011 uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maliasili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahim Musa aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wake Ezekiel Maige.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Capital-Plus International (CPI) ya Dar es Salaam imeandaa mashindano ya riadha ya kilomita 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2011’ yatakayofanyika Septemba 4 mwaka huu Jijini Mwanza.

CPI inafanya mashindano haya kwa mara ya tatu ambapo ya kwanza yalifanyika mwaka juzi (2009) na tunatarajia mbio hizo zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba kuelekea njia tofauti za Jiji la Mwanza na kumalizia katika uwanja huo.

Mashindano haya mwaka huu yamedhaminiwa na Geita Gold Mine, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), New Africa Hotel, Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bank M, MOIL, New Mwanza Hotel, Shirika la Hifadhi ya Wanyapori Tanzania (TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita tunatarajia wanariadha kutoka sehemu mbalimbali nchini pamoja na nchi jirani watashiriki katika mashindano hayo ya aina yake katika ukanda huo wa Ziwa.

Mialiko kwa ajili ya ushiriki wa nchi jirani ipo tayari na itatumwa kupitia vyama vya michezo husika ambavyo ni Jamhuri ya watu wa Congo (DRC), Rwanda,Burundi, Kenya,Uganda na Zambia.

Mashindano haya pamoja na mbio hizo ndefu pia yatahusisha matukio mengine kadhaa ambayo ni  mbio za kilomita 5 kwa wote , mbio za kilomita 3 kwa wazee wa kati ya umri wa miaka 55 na zaidi, mbio za kilomita 3 kwa watu wenye ulemavu na mbio za kilomita 2 kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 7 -10.

CPI imeamua kuendelea kupanua wigo wa ushiriki mwaka huu kutokana na kutambua umuhimu wa michezo kwa rika mbalimbali lakini muhimu zaidi ni mapendekezo tofauti tuliyopokea kupitia wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka jana.

Fomu kwa ajili ya kujisajili zitapatikana Ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, Ofisi za Capital- Plus International Limited- DSM, Makao Makuu ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) Dar es Salaama, Ofisi za RT Mwanza. Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusiana na mashindano haya unaweza kutuandikia

kupitia info@capitalplus.co.tz.

Zaituni Ituja
+255 713 388 758, +255 715 027 892
MRATIBU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad