HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 11, 2011

Fainali za mchezo wa Safari pool katika ngazi ya kimkoa

Mchezaji wa klabu ya Mpo Afrika,Jackson Stephane akiwa katika mchezo wa fainali za mashindano ya Safari Pool kwa ngazi ya kimkoa iliyofanyika jana kwenye club Laure iliopo Keko,jijini Dar.
Mchezaji Damas Modest wa klabu ya Bashuat akifanya vitu vyake katika fainali hizo.

Fainali za mchezo wa Safari pool katika ngazi ya kimkoa imeendelea jana katika mikoa mbalimbali,ambapo zaidi ya mikoa mitano imefanikiwa kuunda timu za mikoa yao

Mashindano hayo yamemalizika katika mikoa ya Shinyanga,Kilimanjaro,Mkoa maaalum wa kimichezo wa Temeke, Tanga,Dodoma na Iringa.

Kukamilika kwa mashindano hayo katika mikoa hiyo kumewezesha kukamilika kwa idadi ya jumla ya mikoa nane ambapo awali ilitanguliwa na Morogoro na Kagera

Washindi katika mashindano hayo kwa mkoa wa Temeke ni Timu ya Mpo Afrika na wa pili ni Bashnet, wakati bingwa wa singo ni Charles Mushi na Mwana dada Madina.

Mkoa wa Tanga Bingwa ni Timu ya Spider na wa pili ni High way club, bingwa wanadada ni Tima Abbas na wanaume ni Sango Jerry anaetokea timu ya spider.

tukumbuke washindi wa Timu bingwa anapata kiasi cha shilingi laki saba na wa pili laki tatu na nusu , huku singo wanaume bingwa laki tatu na nusu na wanawake laki mbili

Katika mashindano ya mwaka huu mikoa yote kila mkoa utaunda kikosi chake ambacho kitaenda kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika mkoani Dodoma kwenye tarehe 27 hadi 30july2011

Fainali za mwaka huu kwa kiwango kikubwa zimekuwa na mkafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na mwitikio wa timu na jamii nzima kwenye mahudhurio ikiwa ni pamoja na namna ya kulivyokuwa na wachezaji wengi wa jinsia ya kike ambapo ni ishara tosha ya kukua kwa mchezo huo nchini Tanzania.

Napenda kutoa rai kwa watanzania na wapenda michezo kiujumla kijitokeza kwa wingi katika fainali za mikoa ili kuweza kujionea namna mchezo wa Pool ulivyopata umaarufu mkobwa na kujizolea sifa kemkem miongoni mwa wapenzi wa mchezo huo nchini, hakuna kiingilio chochote na sambamba na hilo kutakuwa na beer za Safari lager baridi kwa muda wote wa mashindano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad