HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2011

MZEE MWINYI NA MKUU WA JKT WATEMBELEA SABASABA

Rais Msataafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi (katikati) akisikiliza maelezo mafupi jana jijini Dar es salaam kutoka kwa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja(kulia) kuhusu makaa ya mawe yaliyopo nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Gideon Nasari. Rais huyo mstaafu alitembelea banda la NDC wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi Neema Mbuja(katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali S.N.Kitundu (kushoto) na Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) David Basu (kulia) jana jijini dar es salaam mara baada ya kutembelea banda la NDC kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali S.N.Kitundu (kulia) akisikiliza maelezo mafupi jana jijini Dar es salaam kutoka kwa Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) David Basu (kushoto) kuhusu shughuli mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo. Mkuu huyo wa JKT alitembelea banda la NDC wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam.Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO_Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad