Bondia Francis Miyeyusho akisaini hati ya makubaliano ya mpambano, Dar es Salaam jana kati yake na Mbwana Matumla 'Golden Boy' (kushoto), katika mtanange utakaofanyika Oktoba 30, ukumbi wa Diamond Jubilee. Anayeangalia ni Mwanasheria Yasin Membar wa Kampuni ya Mawakili ya Membar Law Attorney na waliosimama nyuma ni Mkurugenzi wa Dar World Link, Moddy Bawazir (kushoto), ambao ni waandaaji wa pambano hilo na Emmanuel Mlundwa, Rais wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST).
Bondia Mbwana Matumla, akisaini hati ya makubaliano ya mpambano, Dar es Salaam jana kati yake na Francis Miyeyusho (kulia) katika mtanange utakaofanyika Oktoba 30, ukumbi wa Diamond Jubilee. Anayeangalia ni Mwanasheria Yasin Membar wa Kampuni ya Mawakili ya Membar Law Attorney na aliyesimama nyuma niMkurugenzi wa Dar World Link, Moddy Bawazir, ambao ni waandaaji wa pambano hilo.
Mabondia Mbwana Matumla (kushoto) na Francis Miyeyusho wakishikana mikono baada ya kusaini mkataba wa pambano kati yao, Dar es Salaam jana, mbele ya Mwanasheria Yasini Membar (wa tatu kushoto) wa Kampuni ya Mawakili ya Membar Law Attorney, Rais wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST), Emmanuel Mlundwa (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar World Link, Moddy Bawazir, ambao ni waandaaji wa pambano hilo.
No comments:
Post a Comment