HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 18, 2011

Bonanza la michezo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wafanyakazi wa Mabenki visiwani Zanzibar

Wachezaji wa timu mchanganyiko wa mabenki yalioopo visiwani Zanzibar wakifurahia baada ya kunyakua kombe kwa kuwasambaratisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mabao 6-5 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar,ikiwa ni siku michezo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wafanyakazi wa Mabenki yaliyopo Visiwani humo..
Mchezaji wa timu ya benki Mohamed Himid (kushoto) akiwania mpira na Hassan Hamad wa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mchezo wa kusisimua uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.Timu ya Benki ilipata ushindi wa Penati 6-5 baada ya kutoka sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.
Naibu Waziri wa Afya na Utibabu, Dk.Sira Ubwa Mamboya (wa pili kulia) akichuana na akina mama kutoka timu mchanganyiko ya mabenki kwenye mchezo wa kufukuza kuku ambao mwana mama kutoka timu ya benki alifanikiwa kumnyakua kuku huyo.Picha na Mdau Martin Kabemba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad