Mshambuliaji wa timu ya Simba,Ulimboka Mwakingwe (kulia) akichuana vikali na kiungo wa katikati wa timu ya Red Sea ya Eritria,Samuel Berhane katika mchezo wa mashindano ya Kagame-Castle Cup uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa.hadi mwisho wa mchezo si Simba wala Red Sea walioweza kuona lango la mwenzake na kufanya matokeo kuwa 0-0.
Mshambuliaji wa timu ya Simba,Rajab Isihaka (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya Red Sea ya Eritria,Temesgen Asefaw wakati wa mchezo wa kumalizia hatua ya mzunguko wa mashindano ya Kagame-Castle Cup uliochezwa leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Nassor Chollo wa Simba akiwazungusha mabeki wa timu ya Red Sea ya Eritria.
Kipa wa timu ya Red Sea ya Eritria,Daniel Goitom akiruka juu kuudaka mpira uliokuwa katika lango lake.
Sehemu ya Mashabiki wa timu ya Simba waliofurika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar kuisapoti timu yao.
No comments:
Post a Comment