Jumuiya ya wanamitandao ya jamii (social networks) nchini inachukua nafasi ya hii kumpongeza mwanahabari mpiganaji mwenzetu Jackson Mmbando (kulia)kwa kupata nafasi ya kupiga mzigo Airtel Tanzania kama bosi wa Mahusiano wa kampuni hiyo ya simu za mikononi.
Jumuiya inakutakia kazi njema na endeleza mahusiano yako mazuri na vyombo vyote vya habari ambavyo umekuwa ukifanya navyo kazi kwa ufanisi toka huko ulikotoka, na ambako pengo lako halitozibika kirahisi.
Waswahili walinena, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Kaka kazi unaiweza!
Waswahili walinena, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Kaka kazi unaiweza!
Kila la kheri wewe na familia yako mpya ya Airtel
Jumuiya ya wanamitandao
Huyu si alikuwa tigo? Airtel washamchukua! Walimchukua Kelvin na sasa huyu! Kweli tigo ni mentoring ground!
ReplyDelete