HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 19, 2011

CHAMA CHA MCHEZO WA POOL TANZANIA (TAPA) CHATANGAZA KUMALIZIKA KWA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIP- 2011 NGAZI YA MIKOA

Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Lager National Pool Championship 2011 ngazi ya mikoa.kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mchezo wa Pool Tanzania,Amos Kafwinga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mchezo wa Pool Tanzania,Amos Kafwinga akizuongea na waandishi wa habari.

Kampuni ya bia nchini TBL kupitia ya Safari Lager kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Pool Tanzania (TAPA) ,Leo imetoa taarifarasmi ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Lager National Pool Championship 2011 ngazi ya mikoa baada ya kumalizika tarehe 17.07.2011 katika mikoa ya Manyara, Mbeya, Mwanza na Kinondoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wa TAPA Amos Kafwinga alisema. ‘’Mashindano yalianza tarehe 31.06.2011 mpaka tarehe 17.07.2011 kwa ngazi za mikoa na kushirikisha vilabu katika mikoa 14. Mashindano yamemaliza kwa kila mkoa washindi kupata zawadi kama zilivyopangwa. 

Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu Bia ya Safari Lager kuweza kufanikisha ngwe hii muhimu ya ngazi ya mikoa kwa ufanisi wa hali ya juu sana kwa kweli Chama na wachezaji wa mchezo wa pool Tanzania wanajivunia Bia ya SAFARI LAGER.

Kwa u[ande wake meneja wa bia ya Safari Bwana Oscar Shelukindo akitangaza zawadi za ngazi ya Taifa mwaka huu alisema “Bia ya Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imeweza kuleta mapinduzi ya kweli katika mchezo huu, hivyo ni dhamira ya bia ya Safari kuendelea kudhamini mashindano haya ya Taifa na mengi mengineyo ya mchezo wa pool hapa nchini. 

Pia aliwapongeza viongozi na wachezaji wote kwa kuweza kufanikisha mashindano haya katika ngazi ya mikoa alisema’’ kwa kweli inatia moyo sana kuendelea kudhamini mchezo huu’’

Meneja huyo wa Bia ya Safari aliongeza kuwa zawadi za ngazi ya Taifa mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 40% kiwango ambacho ni kikumbwa na ni sifa kwa Bia ya Safari na mchezo wa pool. Akiweka wazi aina za zawadi ambazo washindi wa mwaka huu watapata katika ngazi ya Taifa Bw. Oscar alisema kutakuwa na zawadi za pesa taslimu, vikombe, ngao na medali.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA), Isack Togocho; kwa niaba ya Chama Cha Pool Tanzania alitoa shukurani zake za dhati kwa Bia ya Safari Lager kuweza kufanikisha mashindano katika ngazi ya mikoa kwa ubora wa hali ya juu na kuweka mchezo wa pool juu nchini Tanzania. 

Baada ya kusema hayo mwenyekiti Ndugu Isack Togocho alitangaza rasmi fainali za kitaifa DODOMA zitakazoshirikisha timu teule za mikoa 14 na mashindano hayo yatafanyikia katika ukumbi wa KILIMANI kuanzia tarehe 27.07.2011 hadi tarehe 30.07.2011.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad