Mwanamuziki wa Kimataifa tona nchini Zimbabwe,Oliver Mtukuzi akiimba moja ya nyimbo zake katika Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF),lililofunguliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Oliver Mtukuzi akionyesha umahiri wake wa kulicharaza gitaa wakati wa Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF) usiku wa kuamkia leo.
Mwanamuziki wa Muziki wa Asili nchini,Mrisho Mpoto akienda sambamba na Mkongwe Oliver Mtukuzi wakati wa Tamasha la ZIFF linaloendelea katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Mrisho Mpoto na Ismaeel wa Mjomba Band wakiimba moja ya nyimbo zao.
Vijana wa Kundi la B six wa visiwani Zanzibar wakipnyesha umahiri wao wa kuchemza mbele ya umati mkubwa uliofika Ngome Kongwe kushuhudia ufunguzi wa Tamasha la Filamu Zanzibar.
Wageni toka kila kona ya dunia wakiwa katika Tamasha la Filamu Zanzibar.
MWANAMUZIKI wa kimataifa, Oliver Mutukudzi wa Zimbabwe usiku wa kuamkia leo alikonga nyoyo za mamia ya mashabiki waliofurika kwenye uzinduzi wa tamasha la Filamu za nchi za mahajazi maalufu kama ZIFF uliofanyika ndani ya Ngome kongwe, Zanzibar.
Katika shoo hiyo ya ufunguzi, Mutukudzi aliweza kupagawisha kwa kupiga nyimbo zake mbalimbali zilizotamba za zamani na sasa ikiwemo Ndakuvara,Tozeza na Todii,aliweza kuchukua zaidi ya masaa matatu akiimba na kupiga gitaa hali iliyofanya mashabiki kupiga mayowe kuashiria ni mkali katika muziki wa afrika mbali na kuwa na umri mkubwa.
Mbali na Mutukudzi, mwanamuziki wa Mrisho Mpoto nae aliweza kukonga nyoyo kwa mashahiri yake yaiyokuwa kwenye wimbo wa Adela, aliyoimba sambamba na bendi yake ya Mjomba,alikonga hisia za mamia waliofurika kwenye ukumbi hapo ambapo wengi walipiga mayowe ya kumkubali.
Kivutio zaidi ni pale Mutukudzi na Mpoto kusimama jukwaa ambapo Mutukudzi alikuwa anapiga gita na Mpoto alikuwa akitoa mashahiri ambayo yalikuwa yakiisifia Afrika sambambana tamasha hilo , mashabiki walipihga mayowe kuashiria kuwa Mpoto ni yupo matawi ya juu kwa nyimbo zake ndani ya bara la Afrika.








VIVA AFRICA
ReplyDeleteVIVA MUTKUZI
VIVA MPOTO
BY DUNDA