HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 19, 2011

LIBENEKE LA TONE INTERNET RADIO


salam,
 
Natumai ya kua utakua mzima wa njema afya mimi pia niko salama kabisa, kwanza hongera sana wewe na Timu nzima kwa kazi zenu za Blog ikiwa ni pamoja na kutuletea habari mbali mbali za nchini kwetu, Duniani burudani na michezo big na Mwenyezi Mungu akubariki uendelee mbele zaidi wewe pamoja na timu yako nzima ya matukio. 
 
Kwa niaba ya timu nzima yaTone Internet Radio,tulikua tunaomba msaada wako wa kututambulishia Rasmi Libeneke la Radio yawa Tanzania wote popote Duniani, Tunatanguliza shukurani zetu. Asante sana.

JINA LA SITE YA RADIO: TONE INTERNET RADIO
Tunapenda kulitambulisha watanzania wote waishio popote Duniani kwamba kuanzia sasa wanaweza sikiliza Radio kupitia mtandao yani Internet Buree.
 
Tumeona tufanye hivi kwa kutambua kwamba pamoja na kuwa watanzania wengi wapo hapa nchini na wengi wao kwa sasa wanatumia mtandao na wanapenda sikiliza Radio kupitia mtandao, lakini pia tumezingatia na watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi wapate Burudani, Habari na mambo mengine mengi kutoka Tanzania.
 
Kupitia Tone  Internet Radio watakuwa hawajisikii upweke na kuona kama wapo Tanzania. Pia Tone Radio inawapa wasanii wa Muziki wa aina yoyote Tanzania kuleta nyimbo zao hapa studio na sisi kutangaza kazi zao bure kwa kututumia nyimbo zao kupitia toneinternetradio@yahoo.com 
 
Karibuni sana nyote na pia ukisikiliza Radio mwalike  na mwenzako. 
Pia tunapatikana katikaFacebook profile yetu Tanzania Online-Radio 

Tunatanguliza Shukurani Zetu za Dhati na karibuni sana... Tone Internet Radio Pamoja Tutafika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad