Wakati wapangaji wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Upanga, jijini Dar es Salaam wakiiomba serikali iwauzie nyumba hizo kwa gharama ndogo kwa madai kuwa ni maskini, imebainika kuwa wapangaji hao na wengine wanaopanga nyumba za shirika hilo zilizoko katika maeneo mengine, wana kipato kikubwa.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa wapangaji wengi wa nyumba za NHC Upanga na wengine wanaopanga nyumba za shirika hilo zilizoko katika maeneo mengine, wanazikalia nyumba hizo wakati wamejenga nyumba zao kwa ajili ya makazi, lakini wanazipangisha kwa watu wengine na kulipwa kodi.
Baadhi ya wapangaji wa nyumba zizo wakiwemo wa Upanga, wanailipa NHC fedha kidogo za kodi huku wakilipwa fedha nyingi na wapangaji wanaopanga katika nyumba zao walizojenga katika maeneo mbalimbali.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa mpangaji wa NHC Upanga, Mujengi Josephat anayelipa Sh. 151,000 kwa mwezi ana nyumba yake binafsi namba 509 Kitalu 1katika eneo la Msasani Village na anaipangisha kwa Dola za Marekani 600 kwa mwezi.
Mpangaji mwingine wa NHC Upanga, Abdulahaman Gwao ambaye analipa kodi ya Sh. 70,770 kwa mwezi, anamiliki nyumba binafsi eneo la Msasani Village Plot namba 511 Block F, lakini ameipangisha.
Ferdinand Swai anayepanga nyumba ya NHC Temeke kwa kulipa Sh. 55,000 kwa mwezi, anamiliki nyumba namba 283 Block E na kuipangisha kwa Sh. 450,000 hadi Sh. 600,000 kwa mwezi.
Mwingine ni Zetha Narcis Lyimo anayepanga nyumba ya shirika eneo la Upanga, lakini anamiliki nyumba namba 510 Block A eneo la Kimara Temboni na anaipangisha kwa kodi ya Sh. 250,000 hadi Sh. 350,000 kwa mwezi.
Mwingine ni Agness P.A Heri anapanga nyumba ya shirika Upanga kwa kulipa kodi ya Sh.197,000 kwa mwezi, lakini anamiliki nyumba namba 301 Block C iliyoko Msasani Village na anaipangisha kwa Dola za Marekani 600 kwa mwezi.
Nyaraka zinamuonyesha tena mtu huyo kwa jina la Agness Pauline Heri akipanga nyumba ya NHC iliyoko Upanga lakini akiwa anamiliki nyumba iliyoko eneo la viwanda la Mbezi. Nyumba hiyo ni namba 72/2 Block R ambayo anaipangisha kwa Sh. 500,000 kwa mwezi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, amewaasa wapangaji wa shirika hilo wanaomiliki nyumba zao binafsi kwenda kuishi katika nyumba zao walizojenga ili kuwapisha wananchi wasio na makazi kuwa wapangaji wa shirika hilo.
Mchechu alitoa wito huo hivi karibuni kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kuzungumza na wapangaji wa Upanga.
Alisema serikali iliamua kuanzisha NHC kwa madhumuni ya kuwapatia makazi bora wananchi wasio na uwezo wa kujenga makazi ya, lakini baadhi ya wapangaji wana nyumba zao ambazo wanazikodisha kwa bei kubwa.
Alisema yeye kama mkurugenzi mkuu, alistahili kupatiwa mojawapo ya nyumba hizo, lakini kwa kuwa ana nyumba yake Mbezi, aliona haina haja ya kuchukua nyumba wakati kuna Watanzania wengi wanaotaabika kwa kukosa makazi bora.
“Ndiyo maana namwambia mwenyekiti wa kamati yenu ya wapangaji wa Manispaa ya Ilala iliyowasilisha ombi la kutaka kuuziwa nyumba za Upanga, Mzee Mujengi Gwao, kwamba sisi kama shirika tunajua ana nyumba yake Msasani Village anayoikodisha kwa bei ya dola za Kimarekani 600 kwa mwezi wakati katika nyumba zetu mbili alizopanga, moja ya Upanga analipa Shilingi 151,000 kwa mwezi na ile ya Ilala anakoishi mtoto wake analipa Shilingi 70,770,” alisema.
Siri ya wapangaji NHC hii hapa
ReplyDeleteNa Mwandishi wetu

CHANZO: NIPASHE