HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2011

FAINALI ZA SAFARI LAGER POOL KUFANIKA MKOANI DODOMA

Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi wakati alipokuwa akitangaza idadi ya vyuo vilivyotinga hatua ya fainali katika mashindano ya “SAFARI LAGER HIGHER POOL COMPETITIONS 2011” itakayofanyika Juni 4-5 huko mkoani Dodoma.kulia ni Mratibu wa Mashindano hayo,Innocent Melleck.
Mratibu wa Mashindano ya Pool kwa vyuo vya elimu ya juu,Innocent Melleck (kulia) akitangaza zawadi za washindi zitakazotolewa siku hiyo ya fainali.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo wametangaza rasmi vyuo nane vilivyofanikiwa kuingia fainali ya mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo,Meneja wa bia ya Safari Oscar Shelukindo alisema vyuo vilivyofanikiwa kuingia hatua ya fainali ngazi ya kitaifa ni vile vilivyokuwa mabingwa wa mchezo huo ngazi za Mikoa.

Bwana Shelukindo alisema mashindano hayo kwa ngazi za mikoa yamekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa viwango vya uchezaji jambo linaloonyesha kukua kwa kiwango kikubwa kwa mchezo huo katika ngazi za vyuo.

Akivitaja vyuo vilivyofanikiwa kupata tiketi ya kuingia fainali za kitaifa baada ya kuwa mabingwa katika mikoa ni 1.Dar es salaam ni Chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM), 2.Dodoma ni St Johns University.3.Morogoro ni Sokoine University,4.Mwanza ni St Agustine University,5.Iringa ni Ruaha University.6.Mbeya ni Mbeya Institute of Technology.7 Kilimanjaro ni Stefano Moshi Memorial University College(Tumaini University) na Arusha ni Arusha Institute of Accountancy. ambapo fainali za kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa Polisi Jamii kuanzia jumamosi ya june 04,2011 na jumapili june 05,2011.

Maandalizi ya mashindano hayo ngazi ya kitaifa yamekamilika kwa kiwango cha juu ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Hoteli zitakazofikia hizo timu, usafiri wa kutoka mikoanini hadi dodoma na kurejea vyuoni,usafiri wa ndani mkoani Dodoma na fedha za kujikimu kwa wachezaji nane kwa kila chuo.

Kwa Upande wake mratibu wa mashindano hayo Taifa Innocent Melleck alisema mwaka huu katika ngazi ya kitaifa zawadi ni shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000.00),kombe kubwa na medali, mshindi wa pili ni milioni na laki tano (1,500,000.00) mshindi wa tatu milioni na laki tatu (1,300,000.00) mshindi wa nne milioni moja (1,000,000.00) na washindi wa tano hadi wa nane watapata kifuta jasho cha shilingi laki tano (500,000.00) kila chuo. Ambapo upande wa mchezaji mmojammoja mshindi laki tatu (300,000), wapili laki mbili (200,000) mshindi wa tatu laki na nusu (150,000.00) na mshindi wa nne laki moja (100,000.00).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad