HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2011

WAKURUGENZI NA MAMENEJA WA SHIRIKA LA BIMA WAKUTANA KUJADILI HALI YA SHIRIKA HILO

Mkurugenzi wa utawala na fedha( Bima )Bw Justine Mwandu akitoa hotuba katika kikao cha 3 cha mameneja kilichofanyika katika Hotel ya Giraffe Ocean View jijini Dar es salaam hivi karibuni kuhusiana na mafunzo ya mahudhurio ya ndani na nje ya shirika pamoja na kutathimini hali ya biashara ya shirika hilo kwa sasa huduma zake nzuri ukizingatia na madeni ya muda mrefu ya wateja yanaendelea kulipwa mikoani na katika matawi yalioko Dar es salaam, Bw Justine Alisema wateja wawe na imani na shirika maana wateja wetu ndio wafalme na tupo kwa ajili ya kuwahudumia huku tukiboresha utendaji wa kazi za shirika letu,Waliohuthuria katika kikao hicho ni mameneja wakuu wa mikoa na wakurugenzi wakuu
Mkurugenzi wa idara ya masoko na huduma kwa wateja Anne Mbughuni.akichangia mada katika kikao hicho.
Mameneja wakifurahia jambo kwenye kikao cha tatu cha mameneja na wakurugenzi kushoto Anne mbughuni(DFA)Mwanaidi Shemweta Public Relations (wapili)Bunny Ntimba Manager (watatu) na Adelaide Muganyizi Manager,wa mwisho kulia.
Wakurugenzi wakifuatila kwa umakini mada iliyokuwa ikiendelea katika kikao hicho,Mkurugenzi wa Bima Rose Lawa,wa kwanza,Mkurugenzi wa Bima ya maisha na Persion Bw;Herry Machoke.wa pili.Mukurugenzi wa shirika la Bima Bw;Justine Mwandu.wa tatu.
Mameneja pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo nchini wakiwa katika kikao hicho hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wakurugenzi na mameneja wakiwa katika picha ya pamoja.kwenye kikao cha tatu cha shirika la Bima kilichokuwa kikiendelea katika Hotel ya Giraffe jijini Dar es salaam(Picha zote na Philemon Solomon)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad