HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 8, 2011

VODACOM FOUNDATION WATOA MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI UNUNIO,KUNDUCHI

Afisa wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom,(Vodacom Foundation) Grace Lyon akifurahia jambo na mwanafunzi wa darasa la kwanza Jamila Hamis wa shule ya msingi ununio iliyopo kata ya kunduchi wilaya Kinondoni jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi madawadi 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4,wengine ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Afisa Elimu kata ya kunduchi Geradine Ishengoma ,akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio kutunza madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4 waliyopewa msaada na Vodacom Foundation na kukabidhiwa na Afisa wa mfuko huo Grace Lyon,kulia.
Kutoka kushoto Afisa Elimu kata ya kunduchi Geradine Ishengoma ,Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ununio John Maziku wakiangalia uimara wa moja ya dawati kati ya 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 ,yaliyotolewa msaada na Vodacom kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation,(kulia) aliyekabidhi msaada huo Afisa wa mfuko huo Grace Lyon.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo kata ya kunduchi Wilaya ya Kinondoni wakisikiliza jambo kwa umakini kutoka kwa Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 yenye ya zaidi ya Shilingi million 4.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo Kata ya Kunduchi wilaya ya Kinondoni jijini Dares Salaam wakifurahia msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Vodacom Foundation yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 na kukabidhiwa na Afisa wa mfuko huo, Grace Lyon hayupo pichani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad