HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 15, 2011

SBC TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 10 LEO

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Ziad El Halil akizungumzia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kampuni hiyo inayotengeneza soda mbalimbali ikiwepo Pepsi,katika halfa ya kuadhimisha miaka 10 ya mafanikio,inayoendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar.
Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Rashid Chenja akitoa hotuba inayoelezea kwa ufupi kampuni ya SBC Tanzania Ltd,wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kampuni hiyo hapa nchini.
Mabosi wakuu wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu,Ziad El Halil,Mkurugenzi wa Pepsi Cola,Rashid Mahmoud,Mwenyekiti wa Bodi,Faisal El Halil,Mtendaji Mkuu wa SBC,Mike Hunter pamoja na Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Rashid Chonjo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya heshima kwa kuifanikisha kampuni hiyo.hafla hii inaendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar.
Kamati Kuu iliyofanikisha Hafla ya Miaka 10 ya Kampuni ya SBC Tanzania Ltd ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mchana huu.
Shampeini zikifunguliwaa...
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd wakiwa wameshikana mikono na kunyanyua juu ikiwa ni ishara ya umoja na mshikamano.
Msanii wa Ngoma za Asili hapa nchini,Wanne Star akiwasalimia Wafanyakazi wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar mchana huu huku Mshehereshaji katika hafla hiyo,MC Godwin Gondwe a.k.a Double G akimsikiliza kwa makini.
Wanne Star na kundi lake wakifanya mambo yao.
Kekizz na Shampeinzz.
vijana wa Wanne Star wakifanya mambo yao.
Madansa wa Bendi ya FM Academia wakilishambulia jukwaa ipasavyo mchana huu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd wakiyarudi magoma yaliyokuwa yakinogeshwa na bendi ya FM Academia mchana huu.
Mabosi wakuu,Kulia ni Mtendaji Mkuu wa SBC makao makuu,Mike Hunter akifuatiwa na Mwenyekiti wa SBC Tanzania,Faisal El Halil na mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania,Ziad El Halil.
Wafanyakazi wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd toka sehemu mbali mbali hapa nchini wakiwa katika hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 10 ya kampuni yao hiyo inayoendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad