HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 14, 2011

Mwenyekiti wa TA atembelea kampuni ya Computer for Africa

picha ya pamoja wa wakurengenzi na wafanyakazi wa Computer 4 Africa wakiwa na mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka.


URBAN PULSE inawaleta Ziara ya Mwenyekiti wa Tanzania Assocciation Uk Dr Lusingi akifanya ziara ya kutembelea Watanzania wafanyao shughuli mbalimbali hapa England. Dr Lusingu alifuatana na Mjumbe wa Nec Bi Asha Baraka ili naye ajionee na kujifunza wayafanyayo Watanzania UK. Kampuni hii ya Computer 4 Africa inamilikiwa na mjasirimali wa Kitanzaniana aitwae Bw Aseri Katanga. Kampuni hii inajishughulisha na ukusanyaji wa kompyuta zilizotumika, kisha wanazi karabati kuziweka kwenye hali ya kuwa mpya, halafu wanazisambaza Afrika nzima. Kompyuta hizi hupelekwa kwenye mashule, taasisi mbalmbali na idara ya serikali. Kwa upande wa Tanzania zaidi ya shule 100 zimesha faidika na mpango huu
Kwa maelezo zaidi tembelea www.computer4africa.org.uk.

Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akiteta jambo fulani pamoja na wafanyakazi wa computer 4 Africa na Mwenyekiti wa Tanz UK.
Mkurugenzi wa Aset akiangalia moja ya kifaa kinachotumika wakati wa matengenezo
Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akikagua baadhi ya computer zinazosafirishwa na kampuni ya Computer 4 africa.
baada ya kumaliza ziara kutoka kushoto Ndg Katanga, Dr John Lusingu, Frank Eyembe na Asha Baraka.
computer zilizofanyiwa urekebishwaji na matengenezo tayari kwa kuingia Africa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad