Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermans Mwansoko (mwenye suti)akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa niaba ya baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo ambao wako mkoani Mara kuungana na wananchi kuadhimisha Siku ya Utamaduni Duniani ambayo Kitaifa inaadhimishwa katika Manispaa ya Musoma.

Baadhi ya Viongozi na wafanyakazi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakipata maelezo mafupi nje ya jengo lilimo kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuingia.

Afisa Utawala wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Bw. Patrice Warioba (kushoto) akitoa maelezo kwa Baadhi ya Viongozi wa Idara ya Utamaduni, Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kuhusu baadhi ya vifaa alivyopenda kuvitumia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi ya uhai wake vikiwemo vikombe na viatu ambavo vimehifadhiwa ndani ya makumbusho kijijini Butiama.

Afisa Utawala wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Bw. Patrice Warioba (kushoto) akitoa maelezo kwa Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kuhusu zana mbalimbali za jadi alizopewa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na makabila mbalimbali nchini wakati wa uhai wake alipokuwa madarakani kutokana na kuthamini shughuli za utamaduni.

Baadhi ya Viongozi na wafanyakazi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Utawala wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Bw. Patrice Warioba (kushoto) kuhusu vazi la suti alilopenda kulivaa Mwalimu Nyerere enzi ya uhai wake alipokuwa akitekeleza majukumu mbalimbali ya kitaifa ndani na nje ya nchi ambalo sasa limehifadhiwa ndani ya makumbusho kijijini Butiama.

Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Wizara ya Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Afisa Utawala wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere wakionyeshwa baadhi ya maghala ya kuhifadhia chakula yaliyotumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhifadhia Chakula enzi ya uhai wake alipokuwa akijishughulisha na shughuli za kilimo na kupiga vita adui njaa kwa vitendo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Butiama wakicheza ngoza za asili za kabila la wazanaki nje ya jengo la makumbusho ya historia ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Mara na pia kuenzi mchango wa Mwalimu katika kudumisha utamaduni.

Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Wizara ya Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Afisa Utawala wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere wakipanda juu kuelekea katika eneo ambalo hutumika kuwasha Mwenge wa Uhuru, eneo la Mwitongo Butiama. Viongozi na wafanyakazi hao wako mkoani Mara kuushiriki maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duaniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoani humo.

Eneo la juu likionyesha nyumba aliyojengewa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kijijini Butiama.

Hili ni eneo alilokuwa akilitumia baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa shughuli mbalimbali za kilimo na upandaji miti wakati wa uhai wake kijijini Butiama.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
akumbukwa...Kiswahili ya wapi hiyo?
ReplyDelete