HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2011

MAKAMU WA RAIS KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kesho Jumanne ya Aprili Mosi, 2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Ruvuma katika mji wa Songea.

Makamu wa Rais Dkt Bilal anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho hayo ambayo ujumbe wake Kimataifa ni MISITU NI TUNU YA ASILI. Kwa upande wa Tanzani moto ya siku hiyo kwa mwaka huu ni MIAKA 50 YA UHURU, PANDA MITI NA KUITUNZA: HIFADHI MAZINGIRA.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais anatarajia kuzungumzia hali ya Mazingira nchini kwa miaka 50 tangu uhuru, Mazingira ikiwa ni moja ya Idara/Wizara iliyochini ya Ofisi yake.

Sambamba na shughuli hiyo Makamu wa Rais atapata fursa ya kukagua mabanda mbalimbali katika Uwanja wa Majimaji ambapo pia atapata kusikia salamu maalum za Mkoa wa Ruvuma katika maadhimisho hayo ambayo yataambatana na ujumbe kutoka kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad