HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 8, 2011

Wahitimu 24 wathibitishwa katika makabrasha ya taaluma

Na Mwandishi Wetu

Wahitimu wa Zantel ambao walijiunga na Programu ya First Graduate ya Zantel mwaka 2009 walithibitishwa hivi karibuni na kupokea barua zao za ajira.


Shabaha ya programu hiyo ni kuajili Watanzania vijana wenyevipaji ili wajiunge na familia ya Zantel ambayo mtandao wake unazidikupanua siku baada ya siku na wakati huohuo waendeleze ujuzi wao katika fani walizosomea sehemu zao za kazi.


Waombaji 36 kati ya 200 walifanikiwa kujiunga na Programu ya Kwanza ya Uhitimu (First Graduate Program) ya Zantel na kupangiwa kitengo cha Habari na Teknolojia (IT), Idara za Teknolojia na Biashara ni wahitimu 24 walifanikiwa kumaliza mafunzo ya miaka miwili. Kati ya hao wahitimu 15 ni wa Idara ya Teknolojia na wahitimu 9 ni Idara ya Biashara.


Hussain Kunju, Afisa Rasilimaliwatu wa Zantel, anasema programu imeanzishwa kwa ajili ya kuweka ufanisi katika kazi na maendeleo rasmi kitaaluma. “Tunajivunia programu yetu ya mafunzo kwani imevuka matarajio yetu na hii inatokana na wanaopewa mafunzo kufanyakazi kwa bidii.


Tuko makini kuendele na hii programu kuhakikisha tunawapa fursa Watanzania vijana kujifunza, kupata uzoefu na kuchangia maendeleo yas ekta ya mawasiliano ya simu Tanzania,” alisema.


Miezi sita baada ya tarehe yao ya kukodisha, rejeo la mpito lilifanyika ambalo liliwapa wahitimu hao fursa ya kupata nyongeza ya mshahara kwa kuzingatia utendaji wao. Mameneja wao pia walishauriwa kupendekeza nafasi ambazo wahitimu wataweza uzishikilia baada ya kumalizika kipindi cha maendeleo.


“Tulichagua wale wahitimu bora ambao waliweza kuwajibika sawasawa na kutoa mchango mkubwa kwa Zantel. Hii inafanyika baada ya kupata maelezo kutoka kwa mameneja wao na wafanyakazi wenzao.” Kunju alimalizia kusema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad