HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 9, 2011

LIBENEKE LA MTAA KWA MTAA SASA KATIKA MUONEKANO MPYA


Habari Wadau wa MTAA KWA MTAA BLOG,

Napenda kuwafahamisha kwamba Blogu yetu hii imekuja katika muonekano mwingine kama mnavyoweza kuona hivi sasa, Blogu yetu hii imekuja na muonekano mpya ambao pamoja na mambo mengine imeweza kulitokomeza kabisa lile tatizo lililokuwepo la kupata post za nyuma.

Kuna wanaoweza ona kama hakuna mabadiliko kutokana na jinsi inavyoonekana lakini ukweli ni kwamba imebadilika kimuonekano lakini Blogu yetu ni ile ile ya zamani na sasa hivi una uwezo wa kupata kila kitu ambacho hukuweza kukipata wakati ule iwapo unakuwa umechelewa kukiona katika wakati muafaka,unachotakiwa kufanya kwa sasa hivi unaenda katika sehemu iliyiandikwa "KUMBUKUMBU" na unaweza ita mwezi husika na ikishafunguka unaenda chini kabisa ya posts zote upande wa kulia utaona maandishi yaliyoandikwa "Habari Zilizopita" na hapo utaenda mpaka post husika.

Mabadiliko haya yamekuja sio tu kwa kusikiliza maombi yenu wadau kwamba huwa wanakosa uhondo wa siku za nyuma, bali pia ni kwenda na wakati. Hivyo ukiangalia vyema utakuta pia kuna links za facebook na twitter kwa ajili ya kuongeza ufanisi.

Pia tumerahisisha uwanda wa kutoa maoni ambapo sasa ukishabofya neno 'maoni' utapata sehemu ya kumwaga maoni yako bila shida.

Wadau sasa kuweni huru kutoa maoni kwa uhuru 

Aidha,tunaendelea kupokea maoni na mawazo ya namna ya kuiboresha zaidi Blogu yetu hii ya MTAA KWA MTAA ili iweze kuwa bora zaidi na zaidi.

Naomba kutoa shukrani sana kwa wadau kwa kuendelea kuwa na imani nasi katika kuendeleza libeneke. Vile vile shukrani za kipekee ziwaendee kampuni ya MKCT kwa kuendelea kutoa huduma bora kila siku na kuhakikisha Libeneke halilali kabisa.

Ahsanteni sana na Libeneke liendelee kama kawa.

-Othman Michuzi

MTAA KWA MTAA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad