
Timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania wa jijini Mwanza imeibuka na ushindi wa jumla katika Tamasha la Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Soka Bonanza lililowakutanisha mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Barani Ulaya, ambalo limefanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mara baada ya kuwafunga mashabiki wa timu ya Chelsea ya Uingereza. Mashabiki wa timu ya Real Madrid wa jijini Dar es salaam pia walishinda na kuchukua kombe katika bonanza kama hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam hivi karibuni.
kuibuka washindi wa pili katika bonanza la msimu wa dhahabu unaondelea na serengeti soka bonanza jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm kirumba,jijini Mwanza.

Pichani ni Meneja wa uwanja wa CCM-Kirumba Bwa.Tegete akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Real Madrid mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza,kwenye michuano ya mashabiki wa vilabu hivyo,iliyofanyika jioni ya leo jijini Mwanza,Pichani kati anaeshuhudia ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Bwa.Allan Chonjo,kushoto ni Mratibuwa Bonanza hilo Shafii Dauda akiongea machache wakati kombe likikabidhiwa,nyuma ya meneja wa Serengeti ni Mzee Khalfan Ngasa.

Mashabiki mbalimbai wakiwa wamembeba golikipa wa timu ya mashabiki wa klabu yaReal Madrid mara baada ya kupangua mkwaju wa penati ulipigwa na mchezaji wa Chealsea.

Mtangazaji wa Clouds FM jijini Mwanza,Albert Sengo akifanya mahojiano mafupi na mfanyabiashara maarufu wa samaki ndani ya jiji gili,Jack Masamaki ndani ya uwanja wa ccm-kirumba wakati wa msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti ulipokuwa ukifanyika jioni ya leo,ambapo watu mbalimbali walijitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo la Serengeti Fiesta soka Bonanza 2011.


Vyenga vilitawala mchezo.

Timu ya Real Madrid leo imekuwa kifua mbele kwa mara nyingine tena,kwa kuibuka kinara kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti fiesta soka bonanza ndani ya jiji la Mwanza,pichani mchezi wa timu ya Real Madrid akitaka kumtoka mlinda mlango wa timu ya Chelsea.Picha zote na Braza Men
No comments:
Post a Comment