HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 11, 2011

achomwa moto kwa kuzamia south beach



Pichani ni Bwana Lilah Hussen alieungua vibaya mwili mzima akiwa ndani ya Ambulance ya hospitali ya Kigamboni tayari kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuchomwa moto na walinzi pamoja na meneja wa hoteli ya South Beach iliopo kigamboni alipobainika kuwa aliingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.

Na Mdau Pius Micky wa Spoti na Starehe 

Kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Lilah Hussen,amechomwa na moto mwili mzima na walinzi wa Hotel ya South Beach wakishirikiana na Meneja mmiliki wa Hotel hiyo aliejulikana kwa jina moja la Shipata.

Tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana,limetokea jana mchana katika hoteli hiyo. 

Wakiongea na mwahabari wetu, ndugu wa majeruhi huyo wamesema kuwa ndugu yao alifika ufukweni hapo ambapo kila mwisho wa wiki panakuwa na muziki kwa ajili ya kujiburudisha na alipoingia ndipo alipokamatwa na walinzi kwa kutokuwa na alama maalumu ambayo huvaliwa mkononi kwa waliolipa kiingilio cha hotelini hapo (kiingilio ni Tsh. 7,000/- kwa mtu) ndipo walinzi hao walipochukua jukumu la kumpeleka kwa Meneja wa Hoteli hiyo na ndipo meneja huyo alipoamrisha kijana huyo avishwe mipira na kuchomwa moto.

Bwana Lila ambaye kwa sasa kahamishiwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili amesema yeye ni mfanyabiashara ndogo ndogo na mkazi wa Kigamboni na kuwa alikwenda hapo baada ya kuvutiwa na muziki pasi kujua kama hayo yaliyofanyika hapo yangemkuta.

Ndugu wa majeruhi huyu wamefungua kesi katika kituo cha Polisi Kigamboni lakini hadi hivi sasa na kwa masikitiko wanasema bado hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wa tukio hilo kitu ambacho kinazidi kuwasikitisha ndugu hao wa majeruhi.

Ufukwe wa hoteli ya South Beach umekuwa ukijizolea umaarufu kwa michezo ya ufukweni lakini wananchi wa kawaida ambao wanaishi eneo hili wamekuwa wakilalamikia ada kubwa ya kiingilio ufukweni hapo ikiwa ni Tsh. 7,000/- ada ya kuingia tu bila kinywaji.

Hivyo inafanya wakazi wa maeneo hayo watamani kufika mahala hapo lakini kutokana na gharama za kiingilio kuwa kubwa inawabidi waishie kusikia sifa tu toka kwa watu waendao mahala hapo.

Kijana Lilah kwa sasa yuko Hospitali ya Muhimbili akiendelea kupata matibabu kwani hali yake ilikuwa ni mbaya sana.

Jeshi la Polisi mnaombwa kuliangalia swala hili kwa kina na ikiwezekana hatua za haraka za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika waliofanya jambo hili ambalo ni la kinyama kabisa kwani hili si jambo la kulifumbia macho hata kidogo.

4 comments:

  1. Hakika huu ni unyama kabisa haufai kuachiwa bila kuchukuliwa hatua zaidi.Kwani kuna njia nyingi za kuweza kumchukulia kisheria hapa lazima haki itendeke hata kama aliingia bila kulipa,lakini hukumu waliojipa kumpatia ni zaidi ya madai inabidi wawajibishwe kuanzia hao walinzi mpk huyo mmiliki wa hiyo hoteli na wamtibu na kumlipa fidia akipona,na wakiachiwa hivihivi kila kukicha watazidi kuwatesa wananchi,pesa yao isiwe kigezo cha maonevu na unyama kama huu.

    ReplyDelete
  2. i can not beleive it yaani unamchoma mtu kwa ajili ya sh.7000 unyama wa aina gani huu yakowapi maadili yetu ya kidini jamani lakini wakae wakijua watalipa hayo yote walio mtendea huyu kijana hata kama anamakosa kuna sheria angeukumiwa kuchukua sheria mkononi sio haki hata kidogo hao wenyewe waliomchoma wanafanya makosa je na wao wachomwe wakikosa?hayo maumivu anayoyapata sasa ni ya hali ya juu i was plan to go to that hotel this summer whe i visit home i though it's a good hotel but with this impression i won't even try coz i have a 18 year old son if he do some stupid that the punishment he will get forget it!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. INATIA UCHUNGU SANA KUONA UNYAMA KAMA HUU UKO HAPA TZ TENA JIJINI DAR!!!INASIKITISHA SAANNA TUNATAKA KUONA SHERIA KALI NA ZA HARAKA ZINACHUKULIWA KWA HAWA WOTE WAJINGA WALIOMUADHIBU HUYU KIJANA,NA SERIKALI ISIKAE KIMYA TUNATAKA KUONA NA KUSIKIA HATUA ZINAZOCHUKULIWA, NA ASANTE SANA MWANDISHI WA HIZI HABARI KUWEZA KUTUFUMBUA MACHO NA TUNAKUOMBA UFATILIE KWA KINA ILI TUWEZE KUJUWA KILICHOJIRI BAADA YA HAPA NA PIA WEWE NDIO UTAKUWA CHACHU YA HAO KUADHIBIWA NA HUYU KULIPWA HAKI ZAKE ALIVYODHULUMIWA USICHOKE NA USISITE KUFATILIA HATA KWA KOVA NA MANUMBA

    ReplyDelete
  4. sheria ichukue mkondo wake. binadamu tunasahau kwamba hapa duniani runapita tu na kila nafsi itonja mauti. huu ni unyama wa hali ya juu hata kama amefanya kosa hii ni zaidi ya adhabu.huyo muhindi achukulie hatua ikibidi arudishwe kwao na afilisiwe mali zake.how can a he be that arrogant? jamani hela ni mapito tuu..tunasahau kwamba tutakufa na hela tutaziacha...what is 7000 tsh? if the guy could be knowlegable he couldn,t do such a thing. wananchi inabidi tuandame kwa hili jamani? hivi vitendo vimezidi na sheria inabidi ichukuliwe.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad