HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2011

ZAM yafanya kweli kwa wakazi wa makanya

Mkurugenzi wa vijana wa ZAM-Foundation bwana Hassani Ngoma akimkabidhi Diwani wa Kata ya Makanya Mh. Kitanda Selemani Msaada wa Pump kwa niaba ya wananchi wa Makanya-Kimunyu na wanachama wa ZAM-Foundation.
Sehemu ya Msaada wa Pump za Maji za kumwagilia kama zinavyoonekana katika picha.

Na.Mwandishi wetu.

Taasisi ya Kijamii ijulikanayo kama Zainab Mgonja Community Foundation (ZAM-Foundation) inaanza kutimiza ndoto zake kwa kuweza kuwawezesha wana kijiji wa Makanya Kimunyu kwa misaada mbalimbali.

Toka kuanzishwa kwake mwaka 2007 taasisi hiyo imekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwamo kukipatia Kituo Kikubwa cha Afya cha Makanya - Estate misaada ya vifaa kwa mahospitali ikiwamo magodoro ya kulalia wagonjwa, vitanda vya akina mama vya kujifungulia na vifaa mbalimbali vya kimatibabu.

Msaada huo ulitolewa kwa hisani ya Tigo mwaka 2008.

Mwaka huu, ZAM-Foundation kupitia mradi wake wa “Small Scale Irrigation Program” imefanikiwa kupata pump mbili kubwa za kuvuta maji na kumwagilia kwa kuanzia. Msaada huo umetolewa na Ndugu Mohamed Zia (USA) kupita shirika la kimataifa la Broader View Volunteer.

Msaada huo pamoja na mambo mengine utawawezesha wanakijiji kufanya kilimo cha mbogamboga ikiwamo Kabichi, Mchicha, Nyanya na Vitunguu. Kilimo hiki ni rahisi kuweza kumuingizia mkulima kipato.Msaada huo ulikabidhiwa kwa wanakijiji pamoja na Serikali ya Kijiji cha Mgwasi-Makanya tarehe 29. 01,2011. Shirika hili la ZAM-Foundation limeasisiwa na Bi. Fatma Kange Saleh

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad