Na Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI wa Benki ya Exim wametoa vyakula na mahitaji mengine mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh. mil 5.1/= kwa Wahanga wa mlipuko wa mabomu eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Vitu vilivyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na sare za shule kwa wanafunzi mbalimbali walioathirika, unga wa Sembe, Mchele, Unga wa Ngano, Mafuta ya Kula ,Sukari, Chumvi,Maharagwe, Sabuni na Majani ya Chai.
Meneja Masoko Msaidizi Anita Goshashy alikabidhi vitu hivyo kwa niaba ya wafanya kazi wenzake kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki ambapo alitoa rai kwa wafanyakazi wengine kama wao pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia wahanga husika.
Alisema msaada huo ni katika kuthamini utu wa watanzani wenzao waliopatwa na mkasa huo ambao kwa namna moja au nyingine ni nguvu kazi ya taifa hivyo wanapaswa kufarijiwa kwa kuwapa msaada.
“Tumesikitika na kuguswa kwa namna ya kipekee na tukio lililowapata wenzetu nasi kama miongoni mwa wadau tunatoa msaada wetu wa vyakula na vitu vingine na wale waliojeruhiwa tunawaombea wapone haraka,”alisema
Kwa upande wake Mkuu huyo aliishukuru benki hiyo na kuiomba kuongeza tena msaada mwingine kama uwezo utawaruhusu kwani mahitaji bado ni mengi.
“Tunawashukuru kwa jinsi mlivyoguswa na kuamua kujitolea kwa kiasi mlichoweza,lakini bado tunatoa rai kwenu na kwa wadau wengine kujitolea zaidi endapo uwezo unawaruhusu kufanya hivyo kwani mahitaji bado ni mengi”, alisema mkuu huyo.
Benki hii pamoja na msaada huo,imeshatoa mchango wa damu kwa waathirika husika mapema wiki iliyopita ambapo pia hatua hiyo ililenga kuchangia benki ya damu katika hospitali ya Taifa Muhimbili inayohudumia majeruhi wengi zaidi wa majanga mbalimbali yanayotokea nchini .
Tunashukuru sana kwa kutufariji na muwe na moyo wa upendo kama huo kila siku:
ReplyDeleteJana naona ile huruma ya Tanesco imegota, maana giza kuanzia mchana na usiku kucha. Kipindi kama hiki serikali ingelitizama hili kwa uangalifu kwani mahema na mshumaa hamuoni ni kutafuta janga jingine!
Sawa huruma ina mwisho wake, lakini `tuliomba iwe hivyo'...
Umeme kwa sasa ni muhimu sana kwetu!