HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 13, 2011

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA MPANGO WA SAGCOT

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) wenye lengo la kuwainua na kuwawezesha wakulima wadogo wanufaike na shughuli za kilimo hivyo kukuza sekta binafsi. Wanaoshuhudia uzinduzi huo kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri mkuu Bw. Peniel Lymo na Bw. Frank Braeken mwenyekiti wa ukanda wa Mpango wa Kilimo Kwanza.
Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania na Mabalozi wa Nchi mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa sekta ya Kilimo wakiwemo wawakilishi wa mashirika yanayojihusisha na shuguli za kilimo, mabalozi wa nchi wahisani, mashirika binafsi na wakulima wakiwa ndani ya chumba cha mkutano kushiriki uzinduzi wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wenye lengo la kuwainua na kuwawezesha wakulima wadogo wanufaike na shughuli za kilimo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad