HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 13, 2010

TBL yawazawadia vinara wa uonjaji bia za kampuni hiyo

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kulia) akimkabidhi zawadi mbalimbali mshindi wa kwanza wa shindano la kuonja bia, Alex Lwambano wa Clouds Radio katika shindano lililofanyika mwishoni mwa wiki, Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam.
Waandishi wa habari, waliopata ushindi wa kuonja aina mbalimbali za bia, Alex Lwambano wa Clouds Radio (wa pili kushoto), Said Kilumanga wa Magic Fm Radio (wa pili kulia) na Silvan Kiwale wa gazeti la Mwananchi (nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada ya kuzawadiwa katika shindano lililofanyika mwishoni mwa wiki, Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam. Wafanyakazi wa TBL ni Ofisa Uhusiano, Doris Malulu (katikati), Mtaalamu wa Maabara, Tabitha Manyama (kushoto) na Kelvin Nkya ambaye ni Mtaalamu wa upishi wa bia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad