HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 5, 2010

super d kuapata mafunzo ya ngumi BFT

Mkurugenzi wa Kampuni ya Altaf & Company, Zulfiqal Ali (watatu toka kulia) akikabidhi Pesa Taslim shilingi 150,000 kwa Kocha wa mchezo wa Ngumi, Rajabu Mhamila (Super D)kwa ajili ya kwenda kushiriki mafunzo ya Ukocha yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. katikati ni Mke wa mfadhili huyo,Fatuma Zulfiqal na wengine ni wafanyakazi wa Kampuni Hiyo

Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa Ngumi wa klabu ya Ashanti ambaye pia anatoa mafunzo ya kujitegemea Rajabu Mhamila 'Super D' leo amepata msaada wa Shilingi laki 1.5 zitakazomwezesha kushiriki kozi ya siku 10 ya ukocha iliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).

Msaada huo ambao ni wa pili kwa kocha huyo kupewa uliotolewa na mdau wa michezo Zulfiqal Ali kumwezesha Super D kufanikisha malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana baada ya kushiriki kozi hiyo itakayoanza Desemba 14 hadi 24 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pesa hizo Zulfiqal alisema ameamua kufanya hivyo ili kuungana na wadau wengine wa michezo ikiwemo serikali katika kuendeleza michezo.

"Michezo siku hizi hapa nchini ni ajira kwa vijana wetu na ili tuweze kufanikisha zaidi tunatakiwa kuwawezesha walimu kwanza ambao watatoa mwanga kwa wengine ndio maana nimeguswa katika hili na kusaidia.," alisema.

Hata hivyo Zulfiqal amewaomba wadau wengine kujitokeza kuungana na jamii kusaidia kukuza michezo ili kuwawezesha vijana wasio na ajira waweze kujiajili.

Naye Super D alisema anashukuru na kuahidi kuzingatia kozi hiyo siku zote ili aweze kupanua ujuzi ambao utawawezesha kuwasaidia mabondia wanaochipukia hapa nchini.

Awali kocha huyo alipewa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi laki tatu na zaidi kwa ajili ya mazoezi ya mabondia wanaohudhuria mafunzo yanayotolewa na kocha huyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad