Heshima kwenu wakuu,
Tafadhali naomba kupitia blog zenu tuwasaidie watanzania wenzetu ambao hawajui kuwa si ruhusa kiusalama kufanya shughuli yoyote ile chini ya Tanesco Transmission lines.
Nimeambatanisha picha hii ambayo nimeipiga maeneo ya Tabata (Kinyerezi) ambako kuna makazi mengi mapya lakini uvunjaji mkubwa wa sheria hizi umeanza kufanyika. Aidha mamlaka husika, Tanesco ikiwa mojawapo hazijawaelimisha wananchi juu ya hili.
Katika picha hii wananchi hawa wanaendelea kujenga majengo ya biashara na makazi chini ya HT Line.Miaka 5 au zaidi baadaye Tanesco au Tanrods itawabomolea majengo yao.Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi kwa kuwa ni pesa zinatumika hapa.
Aidha Tanesco wanatakiwa kufanya utaratibu wa kuweka alama za kuwataarifu wananchi kutoendelea kujenga.Watu wengi wanapoteza rasilimali zao kutokana na Mamlaka husika hazitoi elimu ya kutosha kwa wananchi na pia zimekuwa kimya uvunjaji wa taratibu.
Asante
No comments:
Post a Comment