Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Programu za Wanawake wa Benki ya Exim, Felister Simba, wakati wa Tamasha la siku nne la Biashara la Wanawake Wajasiriamali nchini lililoanza jana Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Serikali imeipongeza benki ya Exim kwa kuwasaidia wajasiriamali wanawake hapa nchi katika sekta za kilimo na biashara.
Akizungumza Jijini leo, mara baada ya kutembelea banda la benki hiyo kwenye Tamasha la Biashara la Wanawake Wajasiriamali nchini,Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi Joyce Mapunjo, alisema benki ya Exim imekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanawake wajasiliamli hapa nchini.
“Nawapongeza sana kwa huduma zenu nzuri na ninawaomba muendelee kutoa huduma bora kama ambavyo mmekuwa mkifanya”
Alisema benki hiyo imekuwa na program mbalimbali za kuwaendeleza wanawake hapa nchini, jambo ambalo alisema linasaidia kunyanyua uchumi wa nchi yetu.
Naye Felister Simba, Meneja wa Programu za Wanawake wa benki hiyo, alisema kwamba benki yake imekuwa na program za mafunzo kwa wanawake wajasiriamali, lengo likiwa ni kukuza uchumi wao na na nchi kwa ujumla.
“Tumekuwa na programu za kuwafundisha wanawake ujasiriamali na uendeshaji bora wa biashara katika mikoa mbalimbali, lengo likiwa ni kuwapa wanawake uwezo wa kuendesha miradi mbalimbali” alisema
Bi.Mapunjo alisema kwamba ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wanawake wajasiriali hapa nchi umekuwa ukiongezeka kila mwaka.
Alisema ubora wa bidhaa hizo ni bora kuliko zinazoagizwa nje ya nchi na kuwataka walaji kuzinunua ili kuthibitisha hilo.
“Bidhaa zinazosindikwa na kina mama wajasiriamali ni bora kwa viwango ilinganishwa na zinazoagizwa nje ya nchi na hili ninauhakika nalo” alisema.
Alisema serikali inafarijika kuona bidhaa za kina mama zinakuwa na ubora na kwamba juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa ili kuzitangaza bidhaa hizo ikiwamo maonyesho mbalimbali ya kimataifa.
“Kuna nchi moja hapa jirani yetu wanazichangamkia sana bidhaa zetu kwani wanajua kwamba zina ubora wa hali ya juu na kwa hilo ni lazima tujivunie’Alisema.
Maonyesho hayo ya siku nne yameandaliwa na Shirika la Kazi Duniani, chini ya kuenedeshwa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Nchini( TWCC).
No comments:
Post a Comment