
Pichani inaonekana jinsi juhudi zinavyo fanyika kuzima moto huo mkubwa ambao umewaka soko kuu la Uhindini Jijini Mbeya, hata hivyo moto huo umechelewa kuzimika na Kuathiri maeneo ya jirani kutokana na vitendea kazi duni Jijini hapo ikiwemo na kua na Gari moja tuu la zima Moto na pia wananchi Kuto kuwa na Ushirikiano wa kutosha katika kuzima moto.
Mpaka muda huu bado haijafahamika chanzo cha kutokea kwa moto huo,ila tunaendelea kufuatilia kwa makini ili kuweza kupata sababu zilizopelekea kutokea kwa moto huo,tutaendea kujuzana kadri ripota wetu aliopo eneo hilo atakavyokuwa anatuletea taarifa hizo.
Katika tukio hili pia vibaka nao hawakua Nyuma waliendelea kuiba mali mbalimbali sokoni hapo. Jeshi la polisi kwa kutumia magari yao wameendelea kufanya juhudi za kuokoa Mali za waathilika wa Moto huo.
No comments:
Post a Comment