KAMPUNI ya PrecisionAir inayoongoza nchini katika usafiri wa anga ndani ya Afrika, PrecisionAir imetangazwa kuwa Kampuni Bora ya mwaka ya usafiri wa anga ukanda wa Afrika, na Chama cha Wamiliki wa Ndege wa Afrika (AFRAA).
Tuzo hiyo ilipokelewa na mkurugenzi mtendaji na afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Precision Air, Bw. Alfonse Kioko katika mkutano mkuu wa mwaka wa AFRAA uliofanyika Addis Ababa mwisho wa mwezi wa Novemba.
Mapema mwaka huu, Precision Air iliibuka mshindi wa tuzo za uwekezaji katika Jumuia ya Afrika Mashariki kutokana na kutambuliwa kuwa ilikuwa imefanya uwekezaji bora wa mwaka katika eneo la usafirishaji jijini Kampala, Uganda.
Katika miaka michache iliyopita shirika la ndege la Precision limepata tuzo tofauti zikiwemo:
Tuzo ya wakuu wa makampuni (CEOs) ya Kampuni Inayoheshimika Zaidi nchini Tanzania, katika utafiti uliofanywa na Pricewaterhouse Coopers uliohusisha wakuu wa makampuni Afrika Mashariki mwaka 2008/9
Tuzo ya Mkataba Bora wa Afrika 2008 iliyotolewa na Airfinance Journal (jarida la uwekezaji sekta ya usafiri wa anga) kwa mkataba wa dola za Marekani milioni 129 kama mkopo shiriki wa kununua ndege mpya saba
Tuzo ya Ukodishaji Ndege wa mwaka Afrika 2008 iliyotolewa na Jane's Transport Finance magazine kwa ndege hizo saba.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Bw. Alfonse Kioko alisema "muwe na uhakika kuwa hatutaanza kubweteka kutokana na tuzo hizi ila tutazichukulia kama changamoto kufanya kazi kwa nguvu zaidi kufikia matarajio ya wateja wetu."
Wakati huo huo mkuu huyo alizungumzia maendeleo ya kibiashara ya kampuni akisema kuwa kampuni imepata leseni ya utoaji huduma katika viwanja vya ndege (Ground Handling license) iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), na inangoja kupewa nafasi hiyo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ili ianze kazi hiyo.
Alisema pia kuwa ujenzi wa karakana ya kisasa kabisa ya ndege umeanza na unatazamiwa kukamilika mwezi Machi mwakani. Ujenzi wa karakana utagharimu dola za Marekani 5.4 milioni.
Idadi ya abiria waliosafirishwa imeendelea kupanda kwa asimilia 8.4. Katika kipindi cha miezi sita ya kwanza mwaka huu kampuni ilisafirisha abiria 317,391 ikilinganishwa na abiria 292,821kipindi kama hiki mwaka jana.
Mwezi Septemba kampuni ilikamilisha awamu ya kwanza ya mpango wa kuboresha safu ya ndege za kampuni kuwa za kisasa baada ya ndege ya mwisho kati ya zile saba mpya aina ya ATR kupokelewa.

No comments:
Post a Comment