HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2010

KUMBUKUMBU YA DR. FRANK MARTIN ELIA

MAREHEMU DR. FRANK MARTIN ELIA
03/07/1948 - 04/12/2008

Ni miaka miwili kamili leo tangu ulipotutoka ghafla tarehe 4/12/2008 na kutuachia majonzi makubwa sana katika familia.

Japo tunaamini kwamba kimwili haupo nasi lakini bado tunaamini kuwa kiroho upo nasi na maana twasononeka kila tukukumbukapo, tunaamini ya kuwa uko mahala pema mbinguni.

Tunaamini Mungu amekuwashia taa ewe Baba yetu mpendwa,Dr Elia katika giza na mkono wako wa kuume ukimwongoza. Unakumbukwa sana na mkeo Mwl Grace Elia, wanao Martin, Emmanuel na Esther, ndugu, jamaa na watu wote waliokufahamu.

Mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi,milele na milele Amina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad