
Mnunuzi wa picha ya mtoto wa kimasai (mwenye buluu) akikabidhiwa mzigo wale alioununua kwa dola za kimarekani 1,500 katika mnada uliopitishwa kwenye hafla hiyo

Mshindi wa simu ya Nokia na muda wa maongezi wa shilingi 50,000 akikabidhiwa zawadi yake baada ya kushinda bahati nasibu

Mdau akifurahia zawadi ya blender toka Mini Argos aliyoshinda kwenye bahati nasibu

Mama Chacha akiwa na wana UWF baada ya kuzindua tovuti yao

Meza kuu pamoja na wanachama wa UWF na waume zao. Walioketi kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngereja, akifuatiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu na mgeni rasmi Mama Margaret Chacha.

THT band ilikuwepo kutumbuiza.

wana UWF wakifurahia kusikia kwamba milioni 47 zimepatikana katika hafla hiyo.

Wadau wa UWF.
Jumla ya shilingi milioni 47 zimepatikana katika hafla ya kuchangia mfuko wa kusomesha mtoto wa kike (SOMKI) iliyoandaliwa na Unity of Women Friends (UWF), ambao ni umoja wa kinamama 11 ambao unajishughulisha na kusaidia wasichana katika masomo.
Wanachama wa UWF, ambao ni kinamama wanaofanya kazi maofisini huku wengine wakiwa ni wajasiriamali, pia walisherehekea miaka mitano ya umoja wao katika hafla iliyoafana sana katika ukumbi wa Kibo wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam Ijumaa usiku.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkurugenzi mkuu Mama Margaret Chacha, ambaye aliahidi UWF kwamba benki yake itatoa kila aina ya msaada katika kufanikisha azma yao ya kusomesha mtoto wa kike.
Watu mashuhuri wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu, Mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Fedha wa zamani Mama Zakhia Meghji, pamoja na watu mashuhuri kadhaa.
Mama Chacha pia alikata keki na kuzindua tovuti ya UWF yenye lengo la kutangaza shughuli za umoja huo ambao umekuwa mfano wa kuigwa kwa kinamama wenye moyo wa uzalendo.
No comments:
Post a Comment