HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 27, 2010

FBME yatoa msaada leo

Afisa Mkuu wa Huduma kwa wateja wa benki ya FBME, Jovita Francis (wa sita kushoto) akikabidhi msaada wenye thamani ya laki 5 ikiwa ni mgawanyiko wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kama mchele, unga , sukari , mafuta ya kupikia sabuni za kufulia na kuogea pamoja na mafuta ya kupakaa kwa Sista Rita Jose kiongozi wa vituo vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima katika Kanisa Katoliki kurasini jijini Dar es salaam kwa niaba ya kituo cha watoto yatima cha Sanganyigwa B kilichopo Katabuka,Mkoani Kigoma.wengine ni baadhi ya maafisa wa benki hiyo pamoja na masista waliopo katika kituo hicho.
picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa misaada hiyo.
baadhi ya mizigo iliyokuwa ikikabidhiwa kwa kituo hicho ikishushwa katika gari.
Meneja wa benki ya FBME tawi la Dar es Salaam,Haidery Mwinyimvua akipiga ngoma huku Sista Ritha Jose akimpigia makofi kwa kuonyesha utaalamu huo.
baadhi ya wasichana wanaojifunza usista katika kanisa katoriki la Kurasini wakiimba na kupiga ngoma ikiwa ni sehemu ya kuwakaribisha wageni wao waliowatembelea leo.


Na Ripota wetu.

BENKI ya FBME tawi la Dar es salaam leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto wanaishi katika mazingira magumu pamoja na yatima kilichopo mjini Kigoma.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya msaada huo Afisa mkuu wa huduma kwa wateja wa benki hiyo Jovita Francis alisema imekuwa ni kawaida kwa benki hiyo kila ifikapo mwishoni mwa mwaka kutoa misaada katika vituo vya watoto yatima ikiwa na moja ya huduma ya benki kwa jamii.

Msaada huo wenye thamani ya laki 5 ni mgawanyiko wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kama mchele, unga , sukari , mafuta ya kupikia sabuni za kufulia na kuogea pamoja na mafuta ya kupakaa vilipokelewa na sista Rita Jose kiongozi wa vituo vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima katika kanisa katoliki kurasini jijini Dar es salaam kwa niaba ya kituo cha watoto yatima sanganyigwa B kilichopo mjini kigoma .

Akitoa shukrani kwa niaba ya kituo hicho, Sista Rita Jose aliwataka watanzania wenye uwezo wa kuwasaidia watoto hao kwa namna yoyote ile kufanya hivyo kwani ni njia moja wapo ya kuonyesha hisia za upendo kwa watoto hao ambao maisha yao yanategemea misaada zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad