HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2010

Usiku wa Mtanzania kufanyika desemba 3

Mkurugenzi Muendeshaji wa Peacock Hotel,Damas Mfugale akizungumza leo katika uzinduzi wa usiku Mtanzania uliofanyika katika hotel ya Peacock,jijini Dar asubuhi hii.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hotel hiyo,Joseph Mfugale.
Baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza katika usiku huo,wakiwa pamoja na waandaani na wadhamini wakuu wa usiku huo.

**** **** ***** *****

Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.

Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.

Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.

Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad