HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 19, 2010

JIACHIE SHOW IJUMAA HII NOVEMBER 19, 2010 @08:00PM - 10:30pm EST
 
SHOW INCLUDE: WEEKLY TOP 10 SONGS ZA RADIO MBAO
 
TOP 5 YA WATU WALIOHARIBU WIKI HII
 
SPECIAL GUEST INTERVIEW
 
 
Mbwana Alliy Kuongelea Ujasiriamali kwenye Teknolojia! 
KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII Novemba 20, 2010 @ 01:00pm - 02:00pm EST, 3:00pm -10:00pm East African Time
 
Dunia yetu inazidi kuwa ndogo kutokana na maendeleo ya kisayansi, hasa katika teknolojia ya habari. Zaidi ya hayo, Tanzania imefungua mipaka yake kwa makampuni ya nje kuja kuwekeza nchini, kitu ambacho kinapelekea kuwepo kwa ushindani mkubwa wa kibiashara na ukuwaji wa ubora wa bidhaa na huduma zinatolewa kwa mteja wa kitanzania. Lakini mbali na maendeleo hayo, bado kuna malalamiko ya vijana wengi wa kitanzania kukosa ajira. Ni dhahiri kwamba mojawapo ya vijana kujikwamua ni kujitosa kwenye ujasiriamali. 
 
Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Mbwana Alliy ambaye atachangia uzoefu wake katika mambo ya ujasiriamali, hasa katika eneo la teknolojia ya habari (information technology).
 
Mbwana Alliy mtanzania ambaye kwa sasa hivi makazi yake ni Marekani, ambako anajihusisha na mambo ya teknolojia ya habari katika jimbo la California (eneo maarufu la Silicon Valley). Zaidi,  Mbwana ni vmmiliki wa www.yellowmasai.com, tovuti inayojihusisha na masuala ya uwakala wa usafiri na utalii. 
 
Jiunge nasi kwa kupitia hapa:  http://www.radiombao.com  ili usikose uhondo! 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad