Mwanamuziki ambaye pia ni mpiga gitaa maarufu aliyewahi kuwa Mshindi wa pili wa Bongo Star Search mwaka 2008, Rogers Lucas akilicharaza gita lake kwa hisia kubwa usiku huu katika tamasha la ZIFF linaloendelea katika viwanja vya ngome kongwe,kisiwani Zanzibar. Msanii wa Bongo Freva,Sultan King akifanya vitu vyake jukwaani usiku huu ndani ya viwanja vya ngome kongwe,Zanzibar Mmoja kati ya vijana wa kikundi cha sarakasi kiitwacho Stone Town akionesha umahiri wake wa kucheza sarakasi aina ya Capoera katika viwanja vya ngome kongwe usiku huu.Wadau wakifuatilia tamasha kwa umakini mkubwa.kina nanihii nao wakiyarudi magoma baada ya kukolea hapa ngome kongwe. Kikundi cha muziki wa asili toka jijini Dar,Tatu Robo wakilinogesha tamasha la ZIFF.
No comments:
Post a Comment