HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 19, 2010

Mrembo Wa Arusha Anyakua Taji la Miss Kanda Ya Kaskazini 2010

Mshindi wa miss kanda ya kaskazini Gloria mwanga kutoka mkoani Arusha wa pili ni mshindi wa pili wa shindano la miss kanda ya kaskazini Prisca mkonyi kutoka mkoa wa Kilimanjaro huku mshindi wa tatu ni mshiriki kutoka mkoani Tanga Zulekha Mrisho .Washiriki waliobahatika kuingia tano bora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutajwa wakwanza ni Zulekha mrisho wa pili ni Prisca Mkonyi wa tatu Gloria Mwanga wanne Anna kimambo na watano Zahar Suleman.Picha zote na woinde shizza

Na Woinde Shizza,Arusha

Hatimaye Shindano la kumsaka Miss Tanzania kanda ya kaskazinilimemalizika na mkoa wa Arusha bado umenagangania taji la mrembo huyo baada ya mrembo Gloria Mwanga kutoka mkoani hapa kutwaa taji hilo.

Shindano hilo ambalo liliwakutanisha washiriki takribani 12 kutoka katika mikoa minne iliyoko katika kanda ya kaskazini ambayo ni Arusha ,Manyara ,Kilimanjaro na Tanga lilifana pale ambapo wasanii msanii ambaye alibahatika kunyakua ushindi wa BSS wa mwaka jana Peter msechu aliweza kuwafurahisha watu na kibao chake cha Hasira za nini na kufanya usiku huo kun’gara.

Katika shindano hilo ambalo lilikuwa na upinzani mkubwa wa kila mrembo kuwa na sifa ya kuwa miss na kila mshiriki kuw ana mori wakutetea mkoa wake na kutwaa taji ambalo lilikuwa likishikiliwa na mrembo ambaye aliwakilishamkoa wa Arusha Susan Emmanuel ambaye amekaa nalo taji hilo kwa takribani mwaka mmoja sasa.

Mshiriki kutoka katika mkoa wa Arusha Gloria Mwanga alibahatika kutwa taji hilo na kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja na huku akiwa amebahatikakusoma kozi ya utalii ya miaka miwili ambayo inagarimu kiasi cha shilingi milioni mbili pamoja nakuzawadiwa vocha kwa ajili ya kufanya shoping inayogarimu kiasi cha shilingi laki moja huku akipatiwa kozi ya kifaransa itakayo garimu semista mbili .

Kwa upande wa mshindi namba mbili ambayea ametokea mkoa wa Kilimanjaro Prisca mkoanyi yeye amebahatika kuondoka na fedha taslimu shilingi laki sita huku akibahatika kusoma kozi ya kifaransa ya mwaka mmoja na kupewa vocha ya kufanya shooping na mshindi wa tatu ambaye ni Zulekha Mrisho yeye amebahatika kusoma kozi ya kifaransa kwasemist ambili pamoja na kuondoka na kitita cha shilingi laki nne .

Gazeti hili lilizungumza na Hashimu lundenga naye alisema kuwa anawapongeza waandaaji wa shindano hilo kwa kutoa kipaumbele kuwa pa elimu washiriki ambao wameshiriki shindano hilo na pia sio waho tu bali amewapongeza hata wale ambao waliandaa mashindano ya ngazi ya mikoa.

Naye mratibu wa shindano hili ambaye ni Mkurugenzi wa Miss Northern Zone Erasto Jones toka kampuni ya Crown International Entertainment alisema kuwa wamemaa kuwapa warembo hawa zawadi za elimu kwani wandio nyia ya pekee ya kuwakomboa kimaisha na hawataisahau kabisa.

“unajua tumeona tuwape elimu kwani mfano ukampa gari atatumia litaisha na matokeo yake anaeza ata akapata magonjwa kupitia gari hilo hivyo naona tuwape elimu mana ndio njia pekee ya kuwakombo kimaisha”alisema Jones.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad