HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 8, 2010

Rais Jakaya Kikwete Amkaribisha Rais Lula Da Silva Wa Brazil Ikulu Na Sabasaba

Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais Luiz Inacio Lula Da Silva wa Brazil wakitazama vifaa mbalimbali katika Banda la Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya maonyesho ya Mwalimu Nyerere Jijini Dar. Wa kwanza kulia ni Meneja Mkazi wa Brazafric nchini Tanzania Bw. Readou Sakwa.
Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais Luiz Lula Da Silva wakiingia ikulu jijini Dar na kulakiwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kumpokea leo mchana.
Rais Jakaya Kikwete akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma wakati alipomkaribisha Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil(kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais Kikwete akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma wakati alipomkaribisha Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil Ikulu jijini Dar.
Rais Luiz Lula Da Silva wa Brazil akimuangalia Simba dume aliyekaushwa kwa utaalamu na kuwekwa kama pambo katika mlango wa ikulu jijini Dar
Rais Luiz Lula Da silva wa Brazil akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi namba 9
iliyosainiwa na wanasoka wote nyota wa timu ya Brazil
(Picha na Freddy Maro wa Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad